2 Samuel 23:8-39

Mashujaa Wa Daudi

(1 Nyakati 11:10-41)

8 aHaya ndiyo majina ya mashujaa wa Daudi:

Yosheb-Bashebethi,
Yosheb-Bashebethi au Yashobeamu (1Nya 11:11).
Mtahkemoni, alikuwa kiongozi wa wale Watatu; yeye aliinua mkuki wake dhidi ya watu 800, ambao aliwaua katika pambano moja.

9 cWa pili wake alikuwa Eleazari mwana wa Dodai,
Dodai tafsiri nyingine zinamwita Dodo.
Mwahohi. Akiwa mmojawapo wa wale mashujaa watatu, alikuwa pamoja na Daudi wakati waliwadhihaki Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko Pas-Damimu kwa ajili ya vita. Kisha watu wa Israeli wakarudi nyuma,
10lakini yeye alisimama imara akawaua Wafilisti hadi mkono wake ukachoka na ukagandamana na upanga. Bwana akawapa ushindi mkubwa siku ile. Vikosi vikarudi kwa Eleazari, kuteka tu nyara za waliokufa.

11Aliyefuata alikuwa Shama mwana wa Agee, Mharari. Wafilisti walipokusanyika pamoja mahali palipokuwa shamba lililojaa dengu, vikosi vya Israeli viliwakimbia. 12Lakini Shama akasimama imara katikati ya lile shamba. Akalitetea na kuwaua Wafilisti, naye Bwana akawapa ushindi mkubwa.

13 eWakati wa mavuno, viongozi watatu kati ya viongozi thelathini walishuka, wakamwendea Daudi katika pango la Adulamu, wakati kikundi cha Wafilisti kilikuwa kimepiga kambi katika Bonde la Warefai. 14 fWakati huo Daudi alikuwa katika ngome, na kambi ya Wafilisti ilikuwa huko Bethlehemu. 15Daudi akatamani maji, akasema, “Laiti mtu angenipatia maji ya kunywa kutoka kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu!” 16 gBasi mashujaa hao watatu wakapenya katikati ya Wafilisti, wakaenda kuchota maji kutoka kwa kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu, wakamletea Daudi. Lakini Daudi akakataa kuyanywa. Badala yake, aliyamimina mbele za Bwana. 17 h , iAkasema, “Iwe mbali nami, Ee Bwana, kufanya kitu hiki. Je, hii si damu ya watu ambao walikwenda kwa kuhatarisha maisha yao?” Naye Daudi hakuyanywa.

Haya yalifanywa na hao mashujaa watatu.

18 jAbishai ndugu yake Yoabu mwana wa Seruya ndiye alikuwa kiongozi wa hao Watatu. Aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300 ambao aliwaua, kwa hiyo naye akawa na sifa kama hao Watatu. 19Je, hakupata heshima kubwa zaidi kuliko hao Watatu? Alikuwa jemadari wao, ingawa hakuhesabiwa miongoni mwao.

20 kBenaya mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli ambaye alifanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua mashujaa wawili waliokuwa hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni kulipokuwa na theluji na kumuua simba. 21 lPia alimuua Mmisri mrefu mkubwa. Ingawa Mmisri alikuwa na mkuki mkononi mwake, Benaya alimwendea akiwa na rungu. Alipokonya mkuki kutoka mkononi mwa Mmisri na kumuua kwa mkuki wake mwenyewe. 22Haya yalikuwa mambo ya ushujaa ya Benaya mwana wa Yehoyada; naye pia alikuwa maarufu kama wale mashujaa watatu. 23 mYeye aliheshimiwa zaidi ya wale Thelathini, lakini hakujumuishwa miongoni mwa wale Watatu. Daudi akamweka kuwa kiongozi wa walinzi wake.

24 nMiongoni mwa wale Thelathini walikuwepo:
Asaheli ndugu wa Yoabu;
Elhanani mwana wa Dodo kutoka Bethlehemu;
25 oShama, Mharodi;
Elika, Mharodi;
26 pHelesi, Mpalti;
Ira mwana wa Ikeshi kutoka Tekoa;
27Abiezeri kutoka Anathothi;
Mebunai, Mhushathi;
28 qSalmoni, Mwahohi;
Maharai, Mnetofathi;
29 rHeledi mwana wa Baana, Mnetofathi;
Itai mwana wa Ribai kutoka Gibea ya Benyamini;
30 sBenaya Mpirathoni;
Hidai kutoka mabonde ya Gaashi;
31 tAbi-Alboni, Mwaribathi;
Azmawethi, Mbarhumi;
32Eliaba, Mshaalboni;
wana wa Yasheni;
Yonathani
33mwana wa Shama, Mharari;
Ahiamu mwana wa Sharari, Mharari;
34 uElifeleti mwana wa Ahasbai, Mmaakathi;
Eliamu mwana wa Ahithofeli, Mgiloni;
35 vHezro, Mkarmeli;
Paarai, Mwarbi;
36 wIgali mwana wa Nathani kutoka Soba;
Bani, Mgadi;
37 xSeleki, Mwamoni;
Naharai, Mbeerothi, aliyekuwa mbeba silaha za Yoabu mwana wa Seruya;
38 yIra, Mwithiri;
Garebu, Mwithiri;
39 zna Uria, Mhiti.
Jumla yao wote walikuwa watu thelathini na saba.
Copyright information for SwhNEN